PROMO YA SUMU YA WADUDU YA RAID - Arnold Kayanda
Thursday

Mara nyingi umeona Dawa za kuua Wadudu zikitumia Vikatuni katika Matangazo ya TV ili kujitangaza. Mfano utaona Vikatuni vya Mende wakiingia Jikoni wakijivinjari huku na kule hamadi utaona wakipiga Kelele wakitaja Jina la Dawa iwauayo. Matangazo ya namna hii yalianzizwa miaka ya 60 wakati Kampuni inayotengeneza RAID ilipokuja na msemo wao "Raid Kills Bugs Dead|"