UMOJA WA MATAIFA WATIMIZA MIAKA 68 - Arnold Kayanda
Thursday

Leo Umoja wa Mataifa unaadhimisha kutimiza miaka 68 tangu kuanza shughuli zake. Umoja huu ulianzishwa na waliokuwa washindi wa Vita kuu ya pili ya Dunia mwaka 1945 wakati huo zikiwa nchi 51.

Bastola hii ya mfano ifahamikayo kama "knotted Gun" ama "Non-violence" ni maarufu sana Duniani na japokuwa waendao New York hupenda kupiga picha kwenye Liberty Statue lakini Bastola hii in a ujumbe muhimu zaidi kwa Dunia. Bastola hii ilitengenezwa mwaka 1980 na Msanii wa Kiswedi (Sweden) kisha Serikali ikaipatia UN mwaka 1988 mpaka leo inapatikana katika eneo la Jengo la Umoja wa Mataifa. Pamoja na kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa ukisimamia Amani Duniani lakini umekua ukikutana na Changamoto za vita kona mbalimbali za Dunia. Leo wanaadhimisha miaka 68 ikiwa askari wake wameuawa jana huko Mali usiku wa kuamkia leo katika Bomu la kujitoa muhanga.