Dakika chache baada ya kipigo cha aibu ambacho Arsenal ilikipata mbele ya ,
manchester City wachezaji wawili wa washika bunduki toka London Per Mertersecker na Mesut Ozil walionekana wakizozana baada ya Metersecker kutofurahisha na tabia ya Mesut mbel ya mashabiki wa timu yao.
Per Metersecker ambaye msimu huu amekuwa akiingoza Arsenal kama nahodha alionekana akimnyoonshea kidole Ozil kwa kitendo cha kutoka uwanjani bila kuwapungia mashabiki wa Arsenal waliosafiri toka London hadi Manchester kuangalia mchezo huo.
Metesecker akionekana mwenye hasira alionekana akimkaripia Mjerumani mwenzie huku akimuonyeshea ishara ya kidole na sura yake ikionekana wazi kuwa amekereka .
Ozil hakukaa kimya na alijaribu kujibu mapigo kwa kutoa neno ambalo lilitafsiriwa kama tusi huku akimuonyeshea Metesecker ishara ya mikono kabla ya kukaa kimya baada ya kuona beki huyo mrefu akiendelea kumsakama kwa maneno .
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger alichekelea alipoulizwa juu ya ugomvi wa wachezaji wake na alisema kuwa “nategemea wajerumani hawa watamalizana wenyewe, sina haja ya kuingilia kilichotokea “.
Home
»
»Unlabelled
» KIPIGO CHA 6 - 3 KIMESABABISHA KUTOELEWANA KWA WACHEZAJI WA ARSENAL
Saturday