Umoja
wa mataifa umeondoa usaidizi wake katika mpango wa kuwashambulia waasi
mashariki mwa DR Congo baada ya serikali kukataa kuwafuta kazi
majenerali wawili,msemaji wake amesema.
Vikosi
vya umoja wa mataifa havikuweza kujiunga katika mashambulizi kwa kuwa
majenerali hao wanatuhumiwa na unyanyasaji wa haki za
binaadamu,aliongezea.
Mpango huo wa mashambulizi ulilenga kuwapokonya silaha waasi wa FDLR ambao wanaonekana kama tishio la uthabiti wa eneo hili.
Serikali ya DR Congo haijatoa tamko lolote kuhusu hatua hiyo ya umoja wa mataifa.Awali serikali hiyo ilisema kuwa iliwachagua wanajeshi wake hodari kupigana na FDLR,hivyobasi haitachukua amri kutoka kwa umoja wa mataifa.