Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu, Mmarekani Albert Sokaitis mapema wiki hii alijiuzulu kuifundisha Timu ya Tanzania baada ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania kushindwa kuwasafirisha vijana kwenda Marekani kwenye Mafunzo ya Mpira wa Kikapu. Albert alilalamika iweje Shirikisho na Mamlaka husika washindwe kushughulikia Viza na Tiketi ilhali Gharama zote za vijana hao kuishi Marekani zilishalipiwa.
Hapa Albert akiwa na Timu ya Post University kabla hajaja Tanzania na baadae kubwaga Manyanga. Katibu Mkuu wa zamani,Lawrence Cheyo akizungumzia tukio hilo alisema,"Hii ni aibu na fedheha kwa taifa ukizingatia huyu Kocha ambaye alikataa kulipwa Mshahar na Serikali leo ameamua kujiuzulu"
Moja ya Viwanja vya Mpira wa Kikapu Tanzania.


