JOSEPH KONY - Arnold Kayanda
Friday

Huyu ndiye Joseph Kony hapa akiwa na wanae. Mmoja wa Kiume na mwingine wa Kike. Huyu ndiye anaaminika kuwa Gaidi mkuu (sijui kwa kumlinganisha na yupi) lakini amekuwa akisakwa kwa miaka mingi. Hivi sasa inasemekana anaugua ndio maana anataka kujisalimisha lakini wengine wanasema ni mbinu yake tu. Amekimbilia Afrika ya Kati ambako Serikali inaongozwa na Waasi pia. Swali la kujiuliza ni Je! Afika ya kati wakimpata wanaweza kumkabidhi kwa Uganda, huku tukitilia maanani pia kuwa Serikali yao bado haitambuliwi sana? Na hiyo inakuja baada ya Uganda kukataa wazo la kuwakabidhi M23 kwa Congo?