Miss South Africa Rolene Strauss ameibuka mrembo wa dunia wa mashindano ya Miss World 2014, akiwashinda zaidi ya warembo 120 katika shindano lililofanyika jijini London, Uingereza.
Mshindi huyo wa shindano la Miss World 2014 alivikwa taji la
urembo na mshindi wa Miss World 2013, Megan Young kutoka Ufilipino na
kushangiliwa na mshindi wa pili na wa tatu, ambao ni Miss Hungary Edina Kulcsár
na Miss Marekani Elizabeth Safrit. Kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa mtandao wa
Internet, mshindi huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa
shahada ya udaktari na anafurahia kucheza michezo ya golf, netboli na kuendesha
baiskeli na kujisomea vitabu vya burudani na elimu.
Washindi wa tano wa mwanzo katika mashindano ya urembo ya mwaka
huu walikuwa kutoka Uingereza, Marekani, Hungary, Australia na Afrika Kusini.
Shindano la Miss World 2014 pia lilikuwa na mshindano tanzu na
mataji mengi, ambayo yalifanyika kuelekea siku ya fainali kuu.
Kwa mara ya kwanza, washindani watano walitangazwa kuwa Warembo
wa Miss World 2014 wenye Lengo: Washindi hao ni Miss India, Miss Kenya, Miss
Brazil, Miss Indonesia and Miss Guyana.

