Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania,Mheshimiwa Samuel Sitta akiongea Bungeni leo,amesema Tanzania haiyatambui makubaliano ya mkutano wa Marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kwa kuwa makubaliano hayo hayahusiani na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengine wakubwa hao wa nchi hizo tatu walikubaliana kuondoa malipo ya kile kinachofahamika kama Work Permit miongoni mwa wananchi wao. Viongozi wa Tanzania wameendelea kusisitiza kuwa hawajahusishwa katika maamuzi hayo.
Home
»
»Unlabelled
» BUNGENI
Wednesday