PICHA YA AFRIKA MASHARIKI. - Arnold Kayanda
Wednesday

Wafanyakazi wageni miongoni mwa nchi tatu za Afrika Mashariki wameipokea kwa furaha taarifa ya kuwa kuanzia Januari mwakani hawatatakiwa kulipia vibali vya kufanya kazi katika nchi za Uganda,Kenya na Rwanda. Maamuz hayo yamefikiwa baada ya wakuu wa nchi hizo kukutana Jijini Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa vikao kadhaa miongoni mwao.