Kanye West Jumatatu ya wiki hii aliitumia kumvisha Pete ya Uchumba Kim Kardashian. Wataalam wa Madini wamethibitisha kuwa Pete hiyo ni ya uzito wa Carat 15 za Almas kutoka Lorraine Schwartz.
Inaonekana Kim na Kanye hawakuwa tayari kuiweka Picha hii katika mitandao lakini Mtengeneza Nywele wa Kim aliiweka kwenye Ukurasa wake wa Instagram kisha akaifuta lakini alikuwa ameshachelewa kwani wana mitandao walikuwa wameshaichukua kama unavyoiona.