Ingawa wakenya wengi wameendelea kulalamika kuwa Wanajeshi wa Jeshi la Kenya waliiba Mali katika Maduka wakati wa tukio la Westgate Kiongozi Asman Kamama ambaye ni National Security Chairman kwa mara nyingine tena amekuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali ya Kenya wanaowatetea Wanajeshi hao. Akitoa ufafanuzi mapema leo amesema Mifuko waliyoonekana nayo wanajeshi ilikuwa ni mifuko iliyobeba Maji kwa ajili ya wanajeshi hao kukata kiu. Kauli yake hiyo imezidi kuchochea Moto katika Nyasi kavu za hasira za wakenya wanaoona dhahiri kuwa Wanajeshi wanatetewa ilhali Picha zinaonyesha wazi waliiba.
Katika hatua nyingine mtu anayejiita Omary Abdi amesambaza waraka unaoonyesha kuwa yeye alishirikishwa na Magaidi katika mipango ya awali ya kuilipua westgate na alishiriki kuendesha Gari mojawapo la Magaidi hao na akawashusha pale Westgate. Katika waraka huo amewataja baadhi ya watu walioshiriki katika mpango huo lakini moja ya pengine yatakayozua gumzo ni kitendo cha kutaja Cheo cha Amiri Jeshi Mkuu na nduguze katika Waraka wake. Na anamalizia Waraka wake huo kwa kusema, i write this in a good faith. If i may betray someone may allah have mercy on my soul.
Wakenya na wasio wakenya walipoteza ndugu zao na hasa watoto kwa kuwa sehemu ya jengo hilo ilitumika siku hiyo kwa watoto kufanya mashindano ya mapishi. Mwanamuziki Wahu anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuokoa mwanae kwa kuwa asingebadili Ratiba ya kwenda Westagate na kuamua kwenda kwingine yangemkuta kwani alikuwa tarayri akijiandaa kwenda pale.