Japokuwa Waziri wa Mambo ya ndani Joseph Ole Lenku pamoja na viongozi wa kijeshi wa Kenya wameendelea kuwatetea Wanajeshi (KDF) kuwa hawakuiba katika Maduka yaliyoko katika lililokuwa Jengo la Kibiashara la Westgate, picha za CCTV zilizosambaa zinaonekana kwenda kinyume na utetezi huo kwa kuwa zimewaonyesha Askari hao waliotumwa kuwaokoa watu na mali zao wakiondoka na mifuko inayoaminika ilibeba mali za wenyewe. Wafanyabiashara wengi wamelalamika kuwa maduka yao waliyakuta matupu. Swali kutoka PROMO KWANZA kuja kwako mdau ni kuwa kama ungeingia Mlimani City kuokoa watu na ukafanikiwa kuingia kwenye duka liuzalo Vitu vilivyotengenezwa kwa Madini ya Tanzanite na Almas ungeikumbuka Amri ya Mungu ya usiibe au ungeikumbuka ile ya Kiswahili ya Kufa kufaana?
Hapa KDF wakiingia kuokoa.
Mmoja wa Magaidi akizipita Mali huku na kule kama Camera za CCTV zilivyomuona. Wakenya wamebakia wakijiuliza iwapo Magaidi waliuawa na Wananchi hawakutoka na kitu,ni nani aliiba?