MICHAEL JACKSON NA PEPSI - Arnold Kayanda
Thursday

Miaka ya 80 kulikuwa na makundi mawili,wanywaji wa Cocacola na Wanywaji wa Pepsi. Ili kuifanya Cocacola ionekane ni ya zamani na Pepsi ni ya Vijana wa kisasa ndipo alipofuatwa Michael Jackson aliyekuwa kijana wa kisasa wakati huo. Pesa aliyopewa wakati huo hakuna Msanii hata mmoja alikuwa ameifikia,Dola Milioni 5 za Kimarekani.