MOBUTU SESE SEKO KUKU NGBENDU WA ZABANGA - Arnold Kayanda
Tuesday

 Alikuwa Msafi wa Mavazi tangu Ujana mpaka Uzee. Hata mwanae wa Kike YAKI alipoolewa alimnunulia Gauni la Harusi kwa Dola elfu 70 za Kimarekani (Karibia milioni 100 za kiswahili)

 Alikuwa na Marafiki.
 Ujana wake alitumikia Jeshi la Congo na aliwahi kuwa mwandishi wa habari.

 Hata Wazungu walimpa Sikio lao.

 Aliikimbia Zaire baada ya Kabila Mkubwa kuingia Madarakani Kijeshi.

Alipofariki mwaka 1997 huko Rabat, Morocco akiwa na Umri wa miaka 66 akazikwa huko huko. Ukumbuke pia enzi za utawala wake ndiye alitunza mabaki ya mwili wa Rais wa Burundi  Marehemu Habyarimana mpaka siku ya mwisho Mobutu alipoikimbia nchi ndipo mabaki yakachomwa moto kwa imani ya Hindu.  

Pamoja na kuwa inasemekana aliikamua sana Zaire na kuiibia Mali nyingi zinazokadiriwa kufikia Billion 15 za Dola za Marekani ikiwa ni pamoja na kuishi maisha ya anasa sana,huenda hivi karibuni Mabaki ya mwili wa Mzee Mobutu yakarejeshwa Congo ili kupewa heshima ya kitaifa. Zoezi hilo linafuatia katika juhudi za Kabila mtoto kujaribu kuwaunganisha watu wa congo na kuleta umoja wa kitaifa.