Pamoja na kuwa viongozi wa ngazi za juu za kiusalama katika Kenya watetea Wanajeshi kuwa hawakuiba katika Maduka ya Westgate,Picha za CCTV zilionyesha Askari kadhaa wakibeba Mifuko ya Plastiki inayoonyesha kwa namna yoyote walibeba Mali kutoka katika Maduka yaliyokuwa hapo awali chini ya utekaji nyara wa Magaidi waliojitambulisha kama Al Shaabab. Hatimaye baada ya Uchunguzi wawili kati ya wanajeshi hao wamehukumiwa kifungo huku mwenzao mmoja akiendelea kuwa chini ya Uchunguzi. Mkuu wa Majeshi ya Kenya James Karangi amethibitisha.
Home
»
»Unlabelled
» WANAJESHI WAWILI WA KDF WAFUNGWA KWA KUIBA KATIKA MADUKA YA WESTGATE
Tuesday