Wakazi wa Afrika Mashariki wameishauri Uganda kutolifumbia Macho tishio la Kigaidi lililoelekezwa kwa nchi hiyo hasa ikidaiwa kuwa tahadhari kama hiyo ilitolewa kwa Kenya lakini ikapuuzwa na hatimaye likatokea shambulio la Westgate.
Hata hivyo Serikali ya Uganda kupitia viongozi wao wa Kiusalama wamewahakikishia wananchi wa Uganda kuwa Nchi inalindwa ndani pamoja na Mipaka yake huku ikisemekana kuwa Askari waliokuwa katika mapumziko wamerejeshwa kazini ikiwa ni moja ya hatua za kujihami kwa lolote.