Mwandishi wa ITV Ufoo Saro amejeruhiwa kwa Risasi na anayesemwa kuwa ni Mchumba wake kabla ya Mchumba huyo kumuua kwa Risasi Mama Mzazi wa Ufo Saro na kisha kujiondolea uhai wake kwa Risasi pia. PICHA KUTOKA MAKTABA.
Mzee Reginald Mengi,Mkurugenzi wa IPP MEDIA ambayo inamiliki kituo cha Televisheni cha ITV ambacho ndicho Majeruhi wa Risasi Ufoo Saro anakifanyia kazi akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo amesema ni kweli Ufoo amepigwa Risasi lakini anaendelea vema Muhimbili na Madaktari wametaka apumzike huku Uchunguzi ukiendelea.