Kumekuwepo na shutuma nyingi za ufisadi kwa nchi mbali mbali,hii
ndo ripoti kuhusu viwango vya ufisadi.
Nchi ya Afghanistan, Korea ya
Kaskazini na Somalia ndio nchi zinazoonekana kuwa na ufisadi mkubwa zaidi
Dunianu,huku Denmark na New Zealand zikiwa ndio nchi zenye ufisadi zaidi.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya
kila mwaka iliyotolewa leo na Shirika la Kimataifa la kupambana na Ufisadi la
Transparency International. Shirika hilo limesema kuwa kutokana na ukweli
kwamba zaidi ya thuluthi mbili ya nchi zinaghubikwa na ufisadi, ni hali ambayo
itaathiri ukuaji wa uchumi na kukwamisha vita dhidi ya umaskini na mabadiliko
ya tabia nchi.
Kwa mujibu wa Shirika la
Transparency International – TI lenye makao yake mjini Berlin
Ujerumani,linasema karibu asilimia 70 ya mataifa yote ulimwenguni yanafikiriwa
kukabiliwa na “tatizo kubwa” la ufisadi katika sekta ya umma, na hakuna moja
kati ya nchi 177 zilizofanyiwa utafiti mwaka huu iliyopata alama nzuri. Orodha
ya kila mwaka ya TI ndicho kipimo kinachotumiwa zaidi kuangazia ufisadi katika
vyama vya kisiasa, polisi, mifumo ya mahakama na utumishi wa umma, janga ambalo
lina athari juu ya hatima ya maendeleo ya nchi na vita dhidi ya umaskini.
Nchi zilizoorodheshwa katika
nafasi za mwisho ni pamoja na Iraq, Syria, Libya, Sudan na Sudan Kusini, Chad,
Guinea ya Ikweta, Guinea Bissau, Haiti, na Yemen. Nazo nchi zilizofanya vyema
ni Denmark, New Zealand, Luxembourg, Canada, Australia, Uholanzi, Uswisi,
Singapore, Norway, Sweden na Dinland.
Rwanda iliyo katika nafasi ya
49 ulimwenguni imetajwa kufanya vyema katika eneo la Afrika Mashariki ikifuatwa
na Tanzania iliyo katika nafasi ya 111, Kenya katika nafasi ya 136, Uganda
inayokuja katika nafasi ya 140, na Burundi iliyo kwenye nafasi ya 157. Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo iko katika nafasi ya 154 kwenye orodha hiyo.
Heinrich amesema ufisadi
unahusishwa na nchi zinazosambaratika kutokana na migogoro na ambazo serikali
haziendeshwi kikamilifu na hivyo watu ni lazima watumie kila mbinu kuendesha
harakati zao, kupata huduma, kupata chakula na kuishi.
Mtafiti huyo amesema
Afghanistan ambako majeshi mengi ya magharibi yanayoongozwa NATO yanaondoka
mwaka ujao baada ya kuwa nchini humo kwa zaidi ya mwongo mmoja, ni hadithi ya
kutisha Kwa sababu hawajaona mabadiliko yoyote makubwa. Nchi za magharibi
zinawekeza kiasi kikubwa siyo tu katika masuala ya usalama lakini pia
zinajaribu kurejesha mkondo wa sheria, lakini bado utafiti wa miaka ya karibuni
unaonyesha kuwa idadi ya watu wanaotoa hongo bado ni ya juu kabisa ulimwenguni.