Ndege
mbili za kwanza zilirushwa kutoka mji wa mashariki wa Goma ambao mwaka jana
ulikaliwa kwa muda mfupi na waaasi wa kundi la M23.
Ndege
mbili za kwanza zinaundwa na shirika la Italia la Selex ES.
Msaidizi
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kulinda amani Herve
Ladsous ameiambia BBC kuwa ndege hizo zisizo na rubani, zitatumika kama njia
mojawapo ya kufuatilia harakati za makundi yenye silaha na mienendo ya raia
katika eneo la mashariki mwa Congo.
“Tunatakiwa
kuwa na picha halisi ya kile kinachotokea,” amesema.
Amesema
kama watafanikiwa nchini DR Congo, ndege hizo zinaweza pia kutumika katika
maeneo mengine ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa