Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa 2014 kutoka Nigeria Tayo amezawadiwa kiasi cha Dolla 350,000 kutoka kwa bilionea mkubwa wa Nigeria Ayiri Emami baada ya kushindwa kutwaa ushindi huo ambao ulikwenda kwa mshiriki wa Tanzania ambae anafahamika kwa jina la Idris.
Bilionea huyo wa Nigeria amemzawadia Tayo kiasi hicho cha pesa ambacho ni zaidi ya pesa alizopata mshindi wa shindano la Big Brother Afrika 2014 Idrisa Sultan,Ayiri Emami anaamini kuwa Tayo ndiye aliyestahili kuwa mshindi wa shindano hilo na si Idrisa.
Bilionea huyo anaungana na Wanigeria kibao ambao hawajapenda na hawajafurahishwa na ushindi wa Mtanzania katika mashindano ya Big Brother 2014 ambao walionyesha wizi kupitia mitandao ya kijamii wakipinga na kuzungumza vibaya juu ya ushindi wa Idrisa hali ambayo iliamsha hisia tofauti kwa watanzania wengi na wao kuanza kujibu mashabulizi kupitia mitandao ya kijamii huku wengi wao wakimu Attack msanii Davido kwa kuwa yeye aliweka wazi hisia zake juu ya ushindi wa Watanzania akionyesha kutopenda.
Home
»
Entertainment
» Hii ni baada ya ushindi wa Idirisa Tayo nae kuzawadiwa kitita kinono kufidia kushindwa BBA
Tuesday