Wachezaji
hao Nyambe Mulenga, ambaye huchezea klabu ya Zesco United, Changwe Kalale wa
Power Dynamos na Satchmo Chakawa kutoka Green Eagles walikuwa wanakwenda mjini
Lusaka kwa basi ndogo la klabu ya Zesco United.
Basi
hilo liligongana ana kwa ana na gari lengine katika eneo la Kabwe.
Shirikisho
la soka nchini humo lilisema watu kadhaa walijeruhiwa na kwamba Mulenga
alivunjika mguu.
Duru
katika eneo hilo zilisema kuwa dereva wa basi la Zesco alifariki katika eneo la
ajali huku watu wangine watatu waliokuwa kwa gari la pili pia wakifariki.
Klabu
hio imetoa taarifa kuhusu hali ya wachezaji waliohusika na ajali hio pamoja na
maafisa wengine wa klabu waliokuwa ndani ya basi hio.
Mhasibu
wa klabu hio, Lomuthunzi Mbeba, afisa wa mauzo Fusya Bowa, afisa Frank
Chitambala na mwanchama wa kamati Peter Mutale pia walijeruhiwa ingawa
wanasemekana kua katika hali nzuri.
Kalusha
Bwalya, Rais wa shirikisho la soka Zambia, alithibitisha kuwa maafisa
waliojeruhiwa walifikishwa hospitalini na kwamba hali zao zimeimarika.
Wachezaji
walikua wanasafiri kuelekea mjini Lusaka kwa maandalizi ya michuano ya kombe la
mataifa ya afrika 2015. Michuano hio inaanza tarehe 17 Januari nchini
Equatorial Guinea.
Zambia
itacheza katika kundi B pamoja na DR Congo, Cape Verde na Tunisia