Hakimu mkuu Lillian Buchan aliambia Tumuhirwe kwamba alitenda uhalifu ambao hauna hata kisingizio.
Alisema adhabu aliyompa inamtosha kulingana na makosa yake kwa
kumtesa mtoto ambaye hana hatia.
Babake mtoto huyo, Eric Kamanzi alisema aliweka kamera ya siri
nyumbani kwake baada ya kuwa na shauku kumhusu mfanyakazi huyo.
Kanda ya video iliyomuonyesha Jolly akimtendea unyama mtoto,
ilitoka kwenye kamera ambayo Bwana Kimanzi aliweka nyumbani kwake baada ya
kushuku kuwa mtoto wake alikuwa anatendewa unyama na pia baada ya kumapata
mtoto wake akiwa na alama za majeruhi mwilini mwake.
Alimshitaki mwanamke huyo kwa polisi na kisha kuisambaza kanda
hio kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya hukumu kutolewa,Kamanzi alisema: "sio juu yetu
kuamua adhabu anayofaa kupewa Jolly. ''
"tunatumai kuwa hili ni funzo kwa wafanyakazi wengi wa
nyumbani kwamba huwezi tu kwenda kwa nyumba ya mtu na kumtesa mtoto na
kutarajia kuondoka tu kama ulivyoingia. ''