Promo Kwanza inamtambulisha kwenu Mzalendo Mwanariadha Faustin Baha Sulle ambaye aliwahi kukataa kupokea Tuzo ya Ushindi baada ya kutoiona Bendera ya nchi yake ya Tanzania katika Uwanja zilimofanyika Half Marathon Campionships huko Veracruz Mexico. Kijana huyu alikimbia kwa kasi akajikuta katikati ya wazoefu wa mbio hizi Kenya na Ethiopia akapata nafasi ya pili. Aliichukua Tuzo mara baada ya uongozi wa Mshindano hayo walipolazimika kwenda kuleta Bendera ya Tanzania waliyoiazima kwenye Hoteli ya Kitalii jirani na uwanja huo. Hivi sasa kijana huyu anasimamiwa na Mkongwe mtaalamu wa kukimbiza upepo Gida Budai.
Home
»
»Unlabelled
» FAUSTIN BAHA
Saturday
