Serikali kupitia Shirika linalosimamia viwango nchini Tanzania TBS wamepiga marufuku matumizi ya nguo za ndani za mitumba.
Watu wengi hukusanyika katika masoko mijini ili kujinunulia nguo hizi zilizokwisha kutumika. Wanunuzi wanasema nguo za mitumba ni imara na bei yake ni nafuu. Picha hii niliipata katika Soko la Manzese ambapo pia muuzaji wa kiume alikuwa amezivaa Pamba hizo kuhamasisha.

