Watu kadhaa wanashikiliwa mateka na mtu mmoja au zaidi wenye silaha katika mgahawa wa Lindt mjini Sydney, Australia.
Mamia ya Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira eneo
lilipotokea tukio hilo.
Takriban watu watatu wameonekana ndani ya mgahawa wakiwa
wamenyanyua mikono juu wakiwa wameiegesha kwenye dirisha wakiwa wameshika bendera
nyeusi ikiwa na maandishi ya kiarabu.

Mmoja wa waliokuwa ndani ya mgahawa ambao ulivamiwa na watakaji nyara mjini Sydney
Kamishna wa Polisi wa South Wales Andrew Scipione amesema tukio
hilo halichukuliwi kuwa la kigaidi lakini imethibitishwa kuwa kuna mtu mwenye
silaha anayewashikilia mateka watu kadhaa.
Mashahidi wa tukio hilo wamesema walimuona mtu akiwa na begi na
silaha akiingia kwenye mgahawa, polisi wamefunga eneo hilo, barabara na
kuwaondoa watu katika eneo hilo.